BENKI ya Barclays Tanzania (BBT) imetangazwa kuwa mshindi wa
Tuzo ya Benki Bora kwa mwaka 2012 hapa Tanzania. Taarifa hiyo ilitolewa jijini
London, Uingereza, Alhamisi ya Novemba 29 mwaka huu wakati wa hafla ya Tuzo za
Benki ya Mwaka zinazoratibiwa na kusimamiwa na gazeti la Financial Times.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,
Mkurugenzi Mtendaji wa BBT, Bwana Kihara Maina alisema: “Lengo letu ifikapo
mwaka 2015 ni kuhakikisha kila mtu anataka kuja kwetu kwa kupitia kauli mbiu ya
‘Kaweke Pesa Benki’ (Go-to-bank). Heshima hii kubwa kwetu imeletwa na moyo wa
kujitoa wa wafanyakazi kwa kuwahudumia vyema wateja wetu na hivyo kuyarahisisha
maisha yao.”
Bw.Maina aliongeza: “Kwa jumla Tanzania kuna benki 50 na
kuchaguliwa kuwa Benki Bora nchini ni furaha kubwa kwa wanafamiliwa wa Barclays,
wateja na wadau wote. Hii ni kwa kutambua uwekezaji wetu mkubwa tulioufanya
katika biashara ili kutoa huduma bora kwa wateja wetu. Tunawaahidi Watanzania
kuwa tutawekeza zaidi na kutoa huduma za kibenki zinazokubalika duniani.”
Kwa mujibu wa jarida lifahamikalo kama ‘The Banker Magazine’,
Barclays imeshinda tuzo hiyo ya mwaka kutokana na matumizi ya Teknolojia ya
Mawasiliano kama vile uwekezaji katika mfumo wa kazi (workflow
and imaging systems), kuanzisha huduma za bure za ATM, kuanzisha huduma
za kibenki kwa njia ya mtandao, maendeleo katika biashata ndogo ndogo na za
kati (SMEs) na kuongezeka kwa faida mwaka 2010 na 2011.
إرسال تعليق