
Club maarufu ya usiku Afrika Mashariki na kati, Club Billicanas kesho inatimiza miaka 20 tangu kufunguliwa kwa mara ya kwanza chini ya jina hilo hilo mwaka 1992. Kwa mujibu wa mmoja wa wahusika katika klabu hiyo ya usiku, klabu hiyo imeamua kufanya sherehe za kutimiza miaka hiyo 20 sambamba na kituo cha Radio Clouds Fm ambao nao wanatimiza miaka 13 wikiendi hii.
Kabla ya kufunguliwa upya na kupewa jina hilo la Club Billicanas,
kiota hicho kilikuwa kinaitwa Mbowe Club kwani kinamilikiwa na Mbunge wa
jimbo la Hai na Mkuu wa kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe.
Tayari shamra shamra za shrerehe hizo zimeshaanza ambapo Club
Billicanas na Clouds Fm wamekandaa Street Bash, katika eneo la maegesho
ya magari ambapo kutakuwa na jukwaa na Screen kubwa ambapo wasanii
watatoa burudani huku ma DJ wakikupigia nyimbo kwa mtindo wa video na
audio.
Hisia za Mwananchi inapenda kuipongeza menejimenti na uongozi wa Club billicanas
kwa ujumla kwa kutimiza miongo miwili ya kuwapa watanzania na wageni
burudani.
إرسال تعليق