Mtuhumiwa wa ajali ya basi la Msanya Trans lenye namba za usajili T 803
AJV Nisani Bw Rashid Selemani Msanya (35) lililosababisha vifo vya
abiria 1 na kujeruhi wengine 28 akiwa wodini katika Hospitali ya mkoa
wa Iringa baada ya kusomewa mashtaka yake 40 na mahakama akiwa
kitandani
Wagonjwa na ndugu wa wagonjwa waliolazwa katika wodi hilo wakishuhudia
tukio hilo baada ya hakimu mkazi, mwandamizi mfawidhi wa mahakama
ya mkoa wa Iringa Juma Hasan kumaliza kushughuli za kimahakama
Hospitalini hapo
Na Francis Godwin
DEREVA wa basi la Msanya Trans ambalo lilitapa ajali mbaya jumamosi
ya wiki iliyopita na kusababisha vifo vya watu 11 na kujeruhi
wengine zaidi ya 20 katika eneo la Kichakani kwenye barabara kuu ya
Iringa - Mbeya amesomewa mashitaka 40 akiwa wodini katika Hospitali ya
mkoa wa Iringa.
Wakisoma mashtaka hayo leo katika wodi namba 5 Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa ,mbele ya hakimu mkazi ,mwandamizi mfawidhi wa mkoa wa Iringa Juma Hassan wakili wa serikali Adolph Maganda akisaidiwa na msaidizi wake Hamad Magenda alisema kuwa mtuhumiwa huyo katika kesi hiyo namba 90 ya mwaka 2012 ya usalama barabarani anatuhumiwa kutenda makosa hayo Desemba 8 mwaka huu .
Alisema kuwa mtuhumiwa huyo Bw Rashid Selemani Msanya (35) ambae alikuwa ni dereva wa basi hilo la Msanya Trans lenye namba za usajili T 803 AJV Nissan ambalo lilikuwa likitokea Iringa mjini kwenda Usokami wilaya ya Mufindi alisababisha ajali na kupelekea vifo vya watu 11 waliokufa katika ajali hiyo.
Wakili Magande alisema kuwa mtuhumiwa huyo anatuhumiwa kwa makosa 40 ambapo jumla ya makosa 11 ni ya kusababisha vifo na makosa 28 ni ya kusababisha majeruhi na kosa moja kati ya 40 ni kusababisha ajali na kuharibu gari hilo.
Hata hivyo mtuhumiwa huyo amekana makosa yote na kuendelea kuwa chini ya ulinzi wa polisi wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali hiyo ya mkoa wa Iringa akitibiwa majeraha makubwa ya moto ambao unasadikika kutokana na maji ya rejeta ya basi hilo.
Hakimu wa mahakama hiyo mheshimiwa Hassan alimnyima dhamana mtuhumiwa huyo hadi kesi hiyo itakapotajwa tena Desemba 20 mwaka huu na kuwa mtuhumiwa ataendelea kuwa chini ya ulinzi wa polisi katika Hospitali hiyo.

إرسال تعليق