Mwanamuziki
Kofii Olomide akiimba jukwaani na kundi lake katika Onesho
linalofanyiki usiku huu kwenye viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar
es salaam ambapo wageni waalikwa na mashabiki mbalimbali wamefurika
katika viwanja hivvyo , ili waweze kushuhudia shughuli pevu ya
mwanamuziki huyo nguli wa muziki Barani Afrika.
Fullshangweblog na kikozi kazi
chake chote iko katika eneo la tukio ili kukumuvuzishia matukio
yatakayojiri katika viwanja vya Leaders usiku huu moja kwa moja katika
kukupasha habari na kukuburudisha pia.
Mmoja wa wanenguaji wa mwanamuziki Kofii Olomide akifanya vitu vyake jukwaani kama anavyoonekana katika picha.
Kofii Olomide akiimba na mmoja wa waimbaji wake Cindy.
Mwanamuziki
Kofii Olomide akiwa na mmoja wa waimbaji wake wa kike wakipagawisha
mashabiki wa bendi hiyo waliojitokeza kwa wingi katika viwanja vya
Leaders ili kushuhudia kile anachokifanya jukwaani.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Clouds Media Group akizungumza kumshukuru mwanamuziki
Kofii Olomide na mashabiki waliojitokeza kwa wingi katika onesho hilo
kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam.
Vimwana wanenguaji wa mwanamuziki Kofii Olomide wakimwaga mauno kwa kwenda mbele jukwaani katika onesho hilo.
Mwanamuziki
Kofii Olomide akiwa amezungukwa na vimwana hao ambao ni wanenguajia wa
bendi yake huku akiwa katikati yao kama mfalme.
Hapa ni Burudani ya mauno tu kama inavyoonekana madau.
Mashabiki mbalimbali wa mwanamuziki Kofii Olomide wakifuatilia kwa makini wakati mwanamuziki Kofii Olomide akiimba jukwaani.
Mashabiki wa mwanamziki Kofii Olomide wakishangilia kwa furaha wakati mwanamuziki Kofii Olomide akiimba jukwaani.
Mwanamuziki
Kofii Olomide akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya
bia ya Serengeti Bw. Steve Gannon wa pili kutoka kushoto na Mkurugenzi
wa Masoko Bw. Ephraim Mafuru pamoja na wafanyakazi wengine.
إرسال تعليق