Huyu
ndio mwanajeshi Mathew alietangaza uchumba na Ben ambae ni mwanaume
mwenzake ndani ya Ikulu ya Marekani, amesema kwa mara ya kwanza
walikutana Ikulu ndio maana wamepachagua kwa ajili ya kutangaza uchumba
wao.
Stori
ni kwamba mwanajeshi Mmarekani aitwae Mathew Phelps (35) ametangaza
uchumba wa kumuoa mwanaume mwenzake aitwae Ben (26) wakiwa ndani ya
Ikulu ya Marekani anapoishi Barack Obama.
Kwa
mujibu wa ABC ni kwamba mwanaume huyo aliyechumbiwa kabadili jinsia
ambapo Mathew amekaririwa akisema kwamba siku wanakutana walikutania
Ikulu ndio maana wamefanya hilo tukio Ikulu.
Rais
Barack Obama wa Marekani ni miongoni mwa viongozi wa mataifa makubwa
duniani wanaounga mkono ndoa za jinsia moja, aliitoa hiyo kauli nzito
mwaka huu ambapo siku kadhaa baadae rapper Jay Z nae alihojiwa kwenye
kituo cha CNN na kumuunga mkono Obama kwa kusema ndoa za jinsia moja sio
tatizo kwa sababu watu hawafanyi mapenzi yao hadharani.

إرسال تعليق