KAZIMOTO KUCHUKUA NAFASI YA MRISHO NGASSA EL MERREIKH

Baada ya mchezaji Mrisho Ngassa kuingia mitini huku taarifa za kuaminika kutoka kwa vyanzo vilivyo karibu na mchezaji husika na klabu ya Yanga vikisema - Mrisho amekubali kimsingi kujiunga na mabingwa wa Afrika mashariki na kati baada ya mkopo wake utakapoisha katika klabu ya Simba, hivyo dili lake la kujiunga na El Merreikh kuota mbawa - leo hii kuna taarifa kutoka klabu ya Simba kwamba El Merreikh wameonesha nia ya kumtaka nyota Mwinyi Kazimoto kama mbadala wa Haruna Niyonzima ambaye walikuwa wakimtaka lakini ameamua kubaki kwenye klabu yake.

Akizungumza na mtandao chanzo cha habari kutoka Simba kinasema kwamba, kumefanyika mazungumzo ya mwanzo tu na El Merreikh wameonekana kuvutiwa na Mwinyi kwa kuwa walikuwa wanatafuta kiungo baada ya Niyonzima kukubali kuendelea kuichezea Yanga.

"Simba tupo tayari kumuuza Mwinyi Kazimoto kwa sababu klabu yetu inaamini katika kutoa nafasi kwa wachezaji kujiendeleza zaidi. Mazungumzo yanaendelea na kama kila kitu kikiwa sawa basi hivi karibuni Mwinyi atakuwa mchezaji mpya wa El Merreikh."

Post a Comment

Previous Post Next Post