Baada ya mchezaji Mrisho Ngassa kuingia
mitini huku taarifa za kuaminika kutoka kwa vyanzo vilivyo karibu na
mchezaji husika na klabu ya Yanga vikisema - Mrisho amekubali kimsingi
kujiunga na mabingwa wa Afrika mashariki na kati baada ya mkopo wake
utakapoisha katika klabu ya Simba, hivyo dili lake la kujiunga na El
Merreikh kuota mbawa - leo hii kuna taarifa kutoka klabu ya Simba kwamba
El Merreikh wameonesha nia ya kumtaka nyota Mwinyi Kazimoto kama
mbadala wa Haruna Niyonzima ambaye walikuwa wakimtaka lakini ameamua
kubaki kwenye klabu yake.
Akizungumza na mtandao chanzo cha habari kutoka Simba kinasema kwamba, kumefanyika mazungumzo ya mwanzo tu na El Merreikh wameonekana kuvutiwa na Mwinyi kwa kuwa walikuwa wanatafuta kiungo baada ya Niyonzima kukubali kuendelea kuichezea Yanga.
"Simba tupo tayari kumuuza Mwinyi Kazimoto kwa sababu klabu yetu inaamini katika kutoa nafasi kwa wachezaji kujiendeleza zaidi. Mazungumzo yanaendelea na kama kila kitu kikiwa sawa basi hivi karibuni Mwinyi atakuwa mchezaji mpya wa El Merreikh."

إرسال تعليق