
Jana Bongo5 iliweka habari inayomhusu mtanzania aliekereketwa kwa
taarifa ya Maggie Munthali kushiriki mashindano ya kuwania taji la Miss
Afrika USA wakati, yeye akidhani, hawajawahi kuonekana katika
mashindano yoyote ndani ya Tanzania na kumtuhumu ameilaghai Tanzania kwa
kutumia fursa ambayo alitakiwa itumiwe na Miss Tanzania, labda kwa kwa
mtazamo wa watanzania angeiwakilisha vizuri Tanzania kwa kuwa ni chaguo
la watanzania wote.
Baada ya taarifa hiyo kuwafikia walengwa, kamati ya Miss Tanzania
kupitia kwa afisa habari wao, Bwana Aidan Rico wametoa ufafanuzi kwa
watanzania, hasa hasa waishio USA kuhusiana na mrembo Maggie Munthali
aliyeshiriki shindano la Miss Africa USA.
Katika taarifa yake ambayo aliitoa kupitia mtandao wa kijamii wa
Facebook, bibie Maggie aliana safari yake ya kushiriki Miss Tanzania,
kuanzia ngazi ya Kitongoji cha Mzizima mwaka 2005. Na baada ya hapo
alifanikiwa kuinngia Top 3 ya shindano hilo hivyo kupata nafasi ya
kuiwakilisha kitongoji hicho katika ngazi ya kanda ya Ilala kwa mwaka
huo.Mrembo huyo hakupata nafasi ya kuingia katika Fainali za Taifa kwa
mwaka huo 2005. aliishia ngazi ya Kanda ya Ilala.
ufafanuzi huo unaendelea kwa kusema,Kanda ya Ilala kwa mwaka huo
iliwakilishwa na Feza Kessy, Perminda Raj na Lilian Mushi, na mshindi wa
mwaka huo alikuwa NANCY SUMARI ambaye pia alitwaa taji la MISS WORLD
AFRICA 2005.
Katika taarifa hiyo bwana Rico alitabanaisha kuwa, kamati ya Miss
Tanzania haina kipingamizi chochote kwa mrembo huyo kushiriki mashindano
mengine yoyote ya urembo mahali popote pale. Kamati inamtakia kila la
heri mrembo huyo na wengine watakaojitokeza kutangaza jina la Tanzania
katika fani ya urembo.
Tunamnukuu “Hatujui ni vigezo gani walivyotumia hao waandaaji wa
shindano hilo la Miss Africa USA, hadi kumpa Jina / sash ya Miss
Tanzania, lakini tunaimani tu kwamba ni mrembo anayewakilisha Tanzania
ijapokuwa hakuingia katika Fainali za Taifa”. Mwisho wa kunukuu.
Tukiwa kama wadau wa burudani, mitindo, ulimbwende, michezo, muziki
na fani nyingine zinazofanana na sanaa tunapenda kuhitimisha suala hili,
baada ya kuwa limetolewa ufafanuzi.
Chanzo:- Bongo5
Post a Comment