MAPOKEZI YA PHILIP MANGULA YATIKISA MAKAMBAKO AKABIDHI KADI KWA WANACHAMA WAPYA -LIVE

katibu  mwenezi  wa  wilaya ya Mufindi Daud Yassin Kushoto akiangana na makamu mwenyekiti  wa CCM Tanzania  Bara  Philip Mangula mchana  huu baada ya  kufika mpakani  mwa  Iringa na Njombe
Nyimbo  za mapokezi ya Mangula
Makada  wa  CCM  mjini Makambako
Bw  Deo Mnyika Kushoto akiteta  jambo na mbunge  wa Ludewa  Deo  Filikunjombe katika uwanja  wa mkutano mjini Makambako

Makamu mwenyekiti  wa CCM Bara Philip Mangulla wa  pili  kushoto akiwa na viongozi  wa mkoa  wa Njombe leo baada ya  kuwasili uwanja  wa mikutano wa Makambako
Mbunge  wa  jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe (kulia) akimkaribisha makamu mwenyekiti Tazania bara Bw Philip Mangula leo mkoani Njombe
Makamu mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Tanzania bara Bw Philip Mangula amepata mapokezi makubwa katika mji wa Makambako wilaya ya Njombe mkoa mpya wa Njombe baada ya kuwasili mchana huu akitokea jijini Dar es Salaam.

Mangula ambae  amepokelewa  eneo la  saja  mpakani  mwa  mkoa  wa Iringa na Njombe amewasili mjini Njombe  mida ya saa 7 mchana akiwa ameongozana na  viongozi  wa CCM mkoa  wa Iringa  wakiongozwa na mwenyekiti  wa CCM mkoa huo Jescar Msambatavangu na viongozi wa wilaya ya Mufindi  wakiongozwa na katibu  mwenezi  wa wilaya  hiyo Daud Yassin. 

Katika mapokezi hayo mbali ya  kupokelewa  Mangulla amekabidhiwa  zawadi mbali mbali ikiwemo mbuzi na jembe kwa ajili ya  kulimia  huku  wakimwimbia wimbo  wa maalum wa kibena 'Iligimilo na nyingo " (Jembe na Mundu ) ni baba na mama

Post a Comment

أحدث أقدم