![]() |
| Marehemu Siraju Kaboyonga enzi za uhai wake. |
Mbunge wa zamani wa Tabora Mjini kwa
tiketi ya CCM na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi
wa Mifuko ya Jamii (SSRA), Siraju Juma Kaboyonga, amefariki dunia jijini
Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo Desemba 19, 2012.
"Tunasikitika kuwa leo tumeamka tukiwa na majonzi makubwa baada ya kumpoteza mwenyekiti wetu, Siraju Kaboyonga," amesema Sara wakati akiwa katika mahojiano na mtangazaji Godfrey Gondwe wa kituo cha luninga cha ITV leo asubuhi.
Taarifa zaidi zimedai kuwa Kaboyonga alikuwa akisumbuliwa na maradhi na anatarajiwa kuzikwa jijini Dar es Salaam siku ya Alhamisi, kwenye makaburi ya Kisutu.
Enzi za uhai wake wa kuwa mbunge, Kaboyonga alikuwa akionyesha uwezo mkubwa wa masuala ya uchumi, hasa fedha na benki.
Aling'olewa katika nafasi yake ya ubunge wa Tabora Mjini baada ya kushindwa katika kura za maoni ndani ya CCM na mbunge wa sasa wa jimbo hilo na Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage.
Hivi karibuni aligombea pia ubunge wa Afrika Mashariki huku akiomba kura akiwa katika 'wheel chair' baada ya kupata ajali na kushindwa kufuatia kura alizopata kutotosha.
Inna Lillahi Wa Inna Ilaihi Rajjiuun!

Post a Comment