HUYU NDIO MWANAJESHI ALIETANGAZA UCHUMBA KWA MWANAUME MWENZAKE NDANI YA IKULU YA OBAMA


Huyu ndio mwanajeshi Mathew alietangaza uchumba na Ben ambae ni mwanaume mwenzake ndani ya Ikulu ya Marekani, amesema kwa mara ya kwanza walikutana Ikulu ndio maana wamepachagua kwa ajili ya kutangaza uchumba wao.
Stori ni kwamba mwanajeshi Mmarekani aitwae Mathew Phelps (35) ametangaza uchumba wa kumuoa mwanaume mwenzake aitwae Ben (26) wakiwa ndani ya Ikulu ya Marekani anapoishi Barack Obama.
Kwa mujibu wa ABC ni kwamba mwanaume huyo aliyechumbiwa kabadili jinsia ambapo Mathew amekaririwa akisema kwamba siku wanakutana walikutania Ikulu ndio maana wamefanya hilo tukio Ikulu.
Rais Barack Obama wa Marekani ni miongoni mwa viongozi wa mataifa makubwa duniani wanaounga mkono ndoa za jinsia moja, aliitoa hiyo kauli nzito mwaka huu ambapo siku kadhaa baadae rapper Jay Z nae alihojiwa kwenye kituo cha CNN na kumuunga mkono Obama kwa kusema ndoa za jinsia moja sio tatizo kwa sababu watu hawafanyi mapenzi yao hadharani.

Post a Comment

Previous Post Next Post