
Moto mkubwa umetokea katika mji mkuu wa Nigeria Lagos. Taarifa
zinaarifu kuwa moto huo ulianza katika eneo la kuhifadhi baruti na
kisha kuenea kwa haraka katika majengo mengine yaliyo karibu na ghala
hilo. Moshi mkubwa umeenea kote katika kisiwa cha Lagos na wazima moto wanajithidi kuuzima moto huo.
Bado baadhi ya majengo yanaendelea kuteketea.
Mwandishi wa
BBC anasema maafisa wa kuzima moto walikuwa na wakati mgumu kufika eneo
hilo kutokana na idadi kubwa ya watu waliokuwa hapa.
Kwingineko,
maafisa wa usalama Kaskazini mwa Nigeria wanasema watu waliojihami kwa
bunduki wamefyetua risasi na kuwaua watu sita katika kijiji chenye idadi
kubwa ya wakristo.
Msemaji wa
jeshi ameiambia BBC, kuwa washambuliaji hao waliwafyetua risasi waumini
katika kanisa dogo wakati wa ibada ya Krismasi.
Mshambuliaji mmoja amezuiliwa na maafisa wa usalama katika eneo hilo.
Ripoti zaidi zinasema kuwa ulinzi umeimarishwa ili kuwaondoshea wasiwasi wakaazi wa eneo hilo.
Hakuna kundi
lililodai kuhusika na shambulio hilo katika jimbo la Yobe, lakini kundi
lenye itikadi kali za dini ya Kiislamu la Boko Haram limekuwa
likiwalenga Wakristo katika eneo hilo mara kwa mara.
Chanzo - BBC Swahili
Post a Comment