Mapenzi yalipokuwa motomoto.
Wakati wa ugomvi wao wa kila mara.
Elizabeth alivyo leo.
ELIZABETH Rudavsky wa nchini Canada alimuua ‘mumewe’ Angelo
Heddington mwaka 2003 wakati akijihami asiendelee kumshambulia. Ni
baada ya kumuua ndipo alipofahamu kwamba mtu ambaye alikuwa akijifanya
mumewe kumbe alikuwa ni mwanamke aliyekuwa anatumia uume wa bandia.
Tukio hilo limeripotiwa na vyombo vya habari baada ya mlolongo wa
mrefu wa mashitaka dhidi ya Elizabeth, 27, ambaye alimchoma Angelo, 30,
(jina lake halisi lilikuwa Angela) kwa kisu tumboni na alipofikishwa
hospitali madaktari waligundua alikuwa na uume wa bandia katika nguo
zake.
Akisimulia mkasa huo, Eliza, alisema kamwe hajawahi kumwona Angelo
akiwa uchi, na walikuwa wakifanya mapenzi gizani tu ambapo aliwahi
kumwambia pia kwamba kuna mwanamke aliwahi kumchoma moto sehemu zake za
siri kufuatia ugomvi uliotokea kati yao hapo zamani – jambo ambalo
lilidhihirisha kwamba Angelo alikuwa anatumia kiungo hicho bandia wakati
wakifanya mapenzi.
Ugunduzi huo ulionyesha Angelo alikuwa pia akijifanya mwanamke na
mwanamme ambapo aliwafanyia ukatili kila mara ‘wenza’ wake hao. Hayo
yalithibitishwa na watu wengi walioleta ushahidi kwamba mtu huyo aliwahi
kuwa ‘mume’ au mke wao.
Pamoja na kumuua Angelo, mashitaka dhidi ya Eliza, yalitupiliwa mbali
baada ya kuonekana alikuwa anajihami dhidi ya mashambulizi ya ‘mumewe’
huyo.
CHANZO: DAILY MAIL
إرسال تعليق