NAFASI ZA KAZI
DEREVA - NAFASI MOJA
►Awe amehitimu mafunzo ya udereva
katika chuo cha serikali
►Awe na uzoefu wa miaka 10 katika kazi ya udereva akiwa
amefanya katika mashirika mbalimbali, yakiwemo ya umma.
► Awe na leseni ya Daraja C katika
kipindi hicho cha miaka 10
►Awe na rekodi nzuri ya usalama
barabarani
►Muadilifu, mwaminifu na anayefanya
kazi kwa kujituma
►Umri ni miaka 30 hadi 45
► Mshahara mnono.
KATIBU MUHTASI
(SECRETARY) - NAFASI MOJA
► Awe amehitimu mafunzo ya ukatibu muhtasi
► Awe na uzoefu usiopungua miaka minne katika kazi hiyo
► Awe tayari kufanya kazi na kutekeleza kazi kwa wakati
► Muadilifu, mwaminifu na anayefanya kazi kwa kujituma
► Elimu kuanzia Kidato cha IV
► Awe na uwelewa wa kutosha wa Stadi
za Kompyuta (Computer Skills)
► Umri kuanzia miaka 24 hadi 35
► Mshahara mzuri.
► Kituo cha kazi kitakuwa Iringa
mjini.
Maombi yote yaandikwe
kwa: Naibu Mhariri Mtendaji, Daraja Development Limited (Iringa Office),
yakiambatanishwa na vivuli (photocopy) vya vyeti, wasifu (CV) na barua mbili za
wadhamini, pamoja na moja ya Ofisa Mtendaji wa Mtaa, yawasilishwe katika Ofisi
za Daraja, Jengo la NSSF (Akiba), Chumba Namba 309, mjini Iringa kabla ya
tarehe 26/12/2012.

إرسال تعليق