Chama cha Soka cha Zambia (Faz) kimesema
kinakusudia kuikabili Fifa ili iweze kuitambua kazi iliyofanywa na
mshambuliaji Godfrey Chitalu wa nchi hiyo kwa kufunga magoli 107 mwaka
1972.
Hatua hiyo imefuatia Lionel Messi
kutangazwa kuvunja rekodi ya Mjerumani Gerd Mueller ya kufunga magoli
85, ambapo kwa sasa mwanasoka huyo wa Argentina ana magoli 88 kufikia
mwaka huu 2012.
Msemaji wa
chama cha Soka cha Zambia (Faz) Eric Mwanza amekaririwa akiiambia BBC
Michezo kuwa, chama hicho kinazo rekodi za kudhibitisha kazi ya Chitalu,
hivyo kutaka mchango wake katika soka utambuliwe kimataifa.

إرسال تعليق