![]() |
| Stopilla Sunzu (kulia) akiwa na washkaji zake jijini Lusaka, juzi. |
BEKI
nyota wa klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na
timu ya taifa ya Zambia “Chipolopolo”, Stopilla Sunzu amesema kuwa
ameamua kwenda kuichezea klabu ya Reading inayoshiriki Ligi Kuu ya
England na sio Arsenal kwa sababu kocha Arsene Wenger amemueleza kuwa
ni lazima afuatiliwe kwa muda mrefu zaidi kabla ya kupewa mkataba.Beki
huyo mwenye miaka 23, ambaye amepaa kwenda Ghana pamoja na kocha Herve
Renard na Rainford Kalaba kuhudhuria hafla ya kesho ya utoaji wa tuzo
za wanasoka bora wa mwaka za Shirikisho la Soka la Afrika (CAF),
amekaririwa na vyombo vya habari vya Zambia akisema kwamba amepata
mwaliko kutoka Reading na kwamba, safari yake ya kwenda England imeiva.
“Nitasafiri kwenda England baada ya mechi yetu dhidi ya Tanzania lakini sitakwenda Arsenal. Arsenal wanataka nijaribiwe kwanza,” alisema Sunzu kabla hajaondoka kwenda Accra, Ghana jana.”
“Badala yake, nitakwenda Reading ambako nitasajiliwa tu na siyo kufanyiwa majaribio.

IMEHAMISHWA: Kutoka straikamkali.blogspot.com

إرسال تعليق