Mgeni rasmi katika kampeni ya Mradi
wa Upandaji Miti jijini Mwanza, Henry Mongi, akipanda mti wakati wa
kampeni hiyo katika moja ya mitaa ya jiji hilo.Anayeshudia kulia ni
Afisa Ubora wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Caroline Muhonoli na wa
pili kutoka kulia ni Diwani wa Kata ya Mkuyuni, Fasheni Lugo. Mradi huo
umefadhiliwa na Kampuni ya Bia Tanzania
Mgeni rasmi katika kampeni ya Mradi
wa Upandaji Miti jijini Mwanza, Henry Mongi, akipanda mti wakati wa
kampeni hiyo katika moja ya mitaa ya jiji hilo.Anayeshudia kulia ni
Afisa Ubora wa TBL, Caroline Muhonoli na wa pili kutoka kulia ni Diwani
wa Kata ya Mkuyuni, Fasheni Lugo.
Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Steven Kilindo, akifukia udongo kwenye
shimo alilopanda mti wakati wa kampeni ya upandaji miti jijini Mwanza
mwishoni mwa wiki..Wanaoshuhudia katikati ni Meneja Ubora wa kampuni
hiyo, Caroline Muhonoli na nyuma ya Kilindo ni Diwani wa Kata ya
Mkuyunim, Lugo Fashen.TBL imetumia zaidi ya milioni 30 kupanda miti 7000
katika mikoa ya Mwanza,Kilimanjaro na Mbeya. Kwa Mkoa wa Mwanza pekee
imetumia sh. mil. 10 kupanda miti 2600.
Meneja wa TBL Mwanza, Richmondx
Raymond akipanda mti katika uzinduzi wa mradi wa upandaji miti jijini
Mwanza mwishoni mwa wiki, uliofanywa na kampuni hiyo kwa kupanda miti
2600 kando kando ya barabara za Balewa, Kenyatta, machemba na shule za
sekondari Nyamaganana na Nyegezi na Kiwanda cha Bia cha kampuni hiyo.
Diwani wa Kata ya Mkuyuni, ambaye
alimwakilisha Meya wa Jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula , Lugo Fasheni
akipanda mti katika uzinduzi wa mradi wa upandaji miti unaotekelezwa
kwa msaada wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL ), jijini Mwanza mwishoni mwa
wiki. TBL tayari imesaidia kupanda miti 2600 jijini Mwanza.
Afisa Misitu Jiji la Mwanza, Kaombe
Phidelis, akitoa taarifa ya hali ya misitu kwa mgeni rasmi , Henry
Mongi wa pili kutoka kushoto,katika uzinduzi wa mradi wa upandaji miti
jana.Wa kwanza ni Meneja wa kiwanda cha Bia (TBL) Mwanza, Raymond
Richmond na kushoto wa kwanza ni Mkurugenzi wa Uhusiano wa Jamii na
Sheria TBL, Steven Kilindo .
Mmoja wa wanafunzi wa Shule ya
Sekondari ya Nyegezi na mtumishi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),
wakipanda mti kwa pamoja katika shule hiyo, jijini Mwanza juzi. TBL
imetumia zaidi ya milioni 30 kupanda miti 7000 katika mikoa ya
Mwanza,Kilimanjaro na Mbeya. Kwa Mkoa wa Mwanza pekee imetumia sh. mil.
10 kupanda miti 2600
Post a Comment