
Hii
ni mara ya tatu kuandaa TOTO PARTY kwa ajili ya watoto wa jiji la Dar
es Salaam na itafanyika Krismasi na Boxing Day ndani ya Cine Club.
Katika
Tamasha hilo, watoto watapata nafasi ya kushiriki katika michezo
mbalimbali kama soka la ufukweni, kuogelea, kusaka hazina (Treasure
hunt) na kujipaka rangi usoni (Face painting) na mengine mengi.
Aidha watoto hao pia wataweza kufunga akaunti ya benki kwa watoto inayojulikana kama ‘Pambazuka’ kupitia benki ya Ecobank.
Mbali
na watoto kucheza na kufurahi michezo mbalimbali pia wazazi wao
watachuana katika mchezo wa kuvuta kamba ambapo washindi katika michezo
hiyo watazawadiwa zawadi mbalimbali na viingilio ni Sh 3,000 kwa watoto na wakubwa Sh 7,000.
إرسال تعليق