
Wapiganaji wa Al Shabaab sasa wametorokea Kusini mwa Somalia
Maafisa kutoka jimbo
lililojitenga la Puntland nchini Somalia wamesema kuwa wanajeshi kumi na
mbili wa serikali ya Somalia wameuwawa na kundi la wanamgambo wa
kislaamu la Al shabaab katika eneo la milima ya Galgalo
Walisema kulikuwa na mashambulizi mawili tofautio ambapo wanjeshi waliuawa katika eneo la milimani la Galgalo.Kwa mujibu wa taarifa za kundi la Al shabaab waliwauawa zaidi ya wanajeshi 30 wa serikali kabla kutoweka katika milima hiyo.
Wapiganaji wengi wa Al Shabaab wameripotiwa kukimbilia eneo la Puntland katika miezi ya hivi karibuni huku jeshi la Somalia pamoja na wanajeshi wa Muungano wa Afrika kudhibiti Kusini mwa Somalia.
Chanzo:- BBC Swahili
إرسال تعليق