Hoteli
ya Double Tree, iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam, iliyofungiwa na
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, (Mazingira) kutokana na
kushindwa kudhibiti maji machafu yanayotiririka kutoka katika Hoteli
hiyo na kumwagika Baharini bila kujali uchafuzi wa mazingira.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (mazingira) Dkt. Terezya Hivisa
(katikati) akikagua mfumo wa maji taka katika Hoteli ya Double Tree,
iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam, wakati alipofika kufanya ukaguzi wa
mfumo wa maji taka katika hoteli hiyo.
''Haiwezekani,
kwa hali hii tunawafungia ili mjifunze'', Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Makamu wa Rais (mazingira) Dkt. Terezya Hivisa (katikati) akizungumza na
Mkurugenzo Mkazi wa Hoteli hiyo, Karim Kanji (kulia) na kumpa amri ya
kuifunga hoteli hiyo.
Post a Comment