Msanii mahiri wa muziki wa Bongofleva nchini, Ally Timbulo, ameanza
safari mpya kwenye tasnia ya filamu kwa kushoot filamu na Rose Ndauka
akiwa kama ni mhusika mkuu. Filamu hiyo inaitwa World of Benefit.
Ndani ya filamu hiyo Timbulo anakuwa ni kijana anaye onyesha mapenzi
ya kweli kwa Rose aliyeolewa. Waigizaji wengine kwenye filamu hiyo ni
pamoja na Mohamed Olutu ‘Mzee Chilo’, Mama Mjata, Hemed Suleiman ‘Phd’,
na Awadhi Saleh muigizaji anayekuja juu katika tasnia ya filamu nchini.
“Nimepata bahati kufanya kazi na wasanii wakongwe kwahiyo ni kitu cha
kujivunia na pia mimi ni mhusika mkuu kwenye hii filamu ambapo Rose
Ndauka kaolewa katika ndoa ya mke zaidi ya mmoja. Rose yupo nyumba ndogo
kwahiyo nyumba aliyopewa na bwana wake ananiita niishi naye kwakuwa
mimi ni mpenzi wake wa muda mrefu kwahiyo namwonyesha “True Love” na
tunapendana sana na yule bwana wake tunamfahamu kama mwezeshaji wa maisha yetu anasema''Timburo
Filamu ya World of Benefit imetayarishwa na mtayarishaji wa filamu
Hamees Suba ‘Kemikali’ na inaongozwa na Selles Mapunda ‘Director of
Directors’, akisaidiwa na Suleiman Mkangara ‘Striker’ kwa upande wa
upigaji picha wapo wataalamu kutoka Bollywood chini ya kampuni ya
Pilipili Entertainment ya jijini Dar es Salaam.
Picha: Filamu Central
Post a Comment