Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania launda Kamati maalumu kwenda Mtwara

Spika wa Bunge Anne Makinda


Spika wa Bunge bi Anne Makinda amesema kuwa, Bunge limeunda Kamati Maalumu kwenda mkoani Mtwara kutafuta suluhu kuhusu suala la nishati ya gesi asilia inayopatikana mkoani humo katika eneo la Mnazibay katika kijiji cha Msimbati kilichopo wilaya ya Mtwara vijijini, mkoani Mtwara. 
Spika Makinda ameyasema hayo wakati akiahirisha kikao cha Bunge kilichoanza leo Mkoani Dodoma ambapo amesema kuwa, matokeo ya Kamati hiyo Maalumu yatawasilishwa kujadiliwa Bungeni.

Post a Comment

Previous Post Next Post