Spika wa Bunge Anne Makinda |
Spika wa Bunge bi
Anne Makinda amesema kuwa, Bunge limeunda Kamati Maalumu kwenda mkoani Mtwara
kutafuta suluhu kuhusu suala la nishati ya gesi asilia inayopatikana mkoani
humo katika eneo la Mnazibay katika kijiji cha Msimbati kilichopo wilaya ya
Mtwara vijijini, mkoani Mtwara.
Spika Makinda ameyasema
hayo wakati akiahirisha kikao cha Bunge kilichoanza leo Mkoani Dodoma ambapo amesema
kuwa, matokeo ya Kamati hiyo Maalumu yatawasilishwa kujadiliwa Bungeni.
إرسال تعليق