Precision Air, Azam Products na chuo kikuu cha Dar es Salaam UDSM, ni
miongoni mwa makampuni bora 20 ya Tanzania yaliyotajwa kama super
brands kwa mwaka 2013, kwa mujibu wa kampuni ya utafiti ya jijini
London, The Centre for Brand Analysis (TCBA).
Pia kwenye orodha hiyo kwa mujibu wa TCBA, 2013/14 makampuni mengine
ni Vodacom, Mlimani City, National Microfinance Bank (NMB), Coca Cola
na Fanta, na M-Pesa.
Mengine ni Kilimanjaro Drinking Water, Chai Bora, Panadol, Foma Gold,
na Kilimanjaro Music Award.Kwa upande wa vyombo vya habari ITV na
Cloud FM vimeongoza.
Post a Comment