Tarehe 26 tuliandika habari kuhusu Mastaa 10 wanaoweza kuwa
wawakilishi wazuri wa Tanzania katika shindano la Big Brother Africa
2013. Katika majina hayo 10, Wema Sepetu, TID, Lisa Jensen na Fezza
Kessy ndio walionekana kuwavutia wengi.
Leo kupitia ukurasa wetu wa Facebook tumeendesha kura ya maoni ambapo
tumewataka watu wawataje mastaa kati ya hao wanne wanaoweza kuwa
wawakilishi wazuri wa Tanzania. Katika kura hizo zaidi ya 800 TID na
Wema ndio walioongoza kwa kutajwa zaidi.
Baada ya matokeo hayo tumempigia simu TID kumpa taarifa hiyo
aliyoipokea kwa furaha kubwa na kudai kuwa hiyo ni ishara ya jinsi
anavyokubalika kwa mashabiki.Tulipomuuliza kama atafikiria kuchukua fomu
kwaajili ya kujaribu bahati yake, Top in Dar amesema kwakuwa watanzania
wamemtaka afanye hivyo basi ataenda kuchukua.
Tunafanya jitihada kupata msimamo wa Wema pia.Tazama maoni hayo hapa:
Post a Comment