
Michuano ya 29 ya AFCON ikiwa imebakiza siku chache kabla ya kuanza,
huku timu ya taifa ya Ghana ikiwa ni moja ya timu zinazopewa nafasi
kubwa ya kunyakua ubingwa wa michuano hiyo kwa pamoja na timu za Zambia,
Ivory Coast na Nigeria.
Ghana itakuwa ikiongozwa na nahodha Asamoah Gyan, lakini kwa hakika
itakuwa ngumu kumuona mshambuliaji wa zamani wa Sunderland na Udinese
akienda kupiga mpira wa penati ikiwa Black Stars watapata penati.
Sio kwa sababu nyingine yoyote bali binafsi - hayati mama yake mzazi alimwambia asipige.
KutokaBBC:
"Nimeamua kutokupiga penati kwenye mechi za timu ya taifa," Gyan alisema.
"[...] Nilisema miezi michache iliyopita kwamba sitopiga penati, kabla
mama yangu hajafariki mwezi November 2011 aliniambia nisipige penati
tena."Kwanini hayati mama yake alimwambia maneno hayo ambayo
yamelionyesha hakuwa anamuamini mwanae?? Gyan anajibu kwamba penati
aliyokosa katika robo fainali ya kombe la dunia 2010 dhidi ya Uruguay,
ambayo ingeifanya Black Stars kutinga nusu fainali ya WOZA 2010.
Pia katika michuano ya AFCON 2012, Gyan alikosa penati katika mechi ya
nusu fainali dhidi ya Zambia ambayo iliingia fainali na kuifunga Ivory
Coast kisha kubeba ubingwa.
Ingawa mshambuliaji huyo mwenye miaka 27 anaweza akalazimika kupiga
penati ikiwa timu yake itakwenda katika hatua ya kupigiana penati ili
kuamua mshindi.
إرسال تعليق