![]() |
| Athumani Kilambo akiingia kwenye gari kurejea nyumbani mara baada ya kuruhusiwa kutoka kwenye Hospitali ya Ocean Road jijini Dar Es Salaam |
Kocha na mwanzilishi wa Pan African ya jijini Dar Es Salaam Kilambo Athumani anasumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya koo,
‘ nasumbuliwa na
kansa ya koo takribani miaka miwili sasa,nimekuwa nikija hapa mara kwa
mara kwa ajili ya kupoza makali tu’ hayo ni maneno ya Kilambo mara baada
ya kupewa ruhusa ya kuondoka kwenye hospitali ya Ocean Road ya jijini
Dar Es Salaam hii leo,
Kilambo amewaomba
wadau wa michezo mbali mbali kujitokeza kwa wingi na kumsaidia hasa
katika kipindi hiki kigumu kumchangia kwa hali na mali ili aweze
kutibiwa ugonjwa huu unaomsumbua na kuhatarisha maisha yake kwa muda
sasa,
‘ Wakati Pan
African tunaianzisha mnamo mwaka 1976 lengo kubwa lilikua ni kuanzisha
klabu kwa ajili ya kusaidiana wakati wa shida na raha,suala la
kuianzisha timu ya mpira lilikuja baadae,wakati ule umoja wetu ulikua na
nguvu sana kiasi kwamba wakati wa matatizo na raha tulikuwa sote,sasa
nawaomba wadau wa michezo hasa wachezaji wa zamani kukumbuka enzi zetu kwa kusaidiana pia kipindi hiki ’ alimalizia kusema ndugu Kilambo.
Miongoni mwa waanzilishi wa klabu ya PAN AFRICAN ni mkurugenzi mtendaji wa
mfuko wa Taifa wa hifadhi ya jamii wa NSSF,Dr Ramadhani Dau, marehemu
Sam Dee,Mzee Ally Abbas,Shiraz Sharrif,Mzee Paul Sozigwa, Dr William
Ugundo na wengineo wengi
Baadhi ya wachezaji waanzilishi wa Pan African ni
Omary Kapera,Adolf Rishard,Jellah Mtagwa, Mohamed Mkweche,Sunday Manara
na Kitwana Manara,Kassim Manara na MAREHEMU Muhaji Mukhi,

Mwanachama wa Pan African Ndugu Yahya ambaye amekuwa naye bega kwa bega kuhakikisha anapona maradhi yanayomsumbua.

Hapa nipo na Mzee Kilambo nilipomtembelea Hospitalini kabla ya kuruhusiwa.
Shaffihdauda blog
Shaffihdauda blog

إرسال تعليق