AZAM FC WAZIDI KUISOGELEA YANGA LIGI KUU - WALIPIGA TOTO LAO 3-1 CHAMAZI LEO HII

Azam FC imeendelea kuipumulia Yanga inayoongoza ligi baada ya leo jioni kuipiga mabao 3-1 Toto Africans ya Mwanza katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Mabao ya Azam katika mchezo huo yamefungwa na Kipre Michael Balou wa Ivory Coast, Brian Umony  na bao la tatu liliwekwa kimiani na Mkenya Humphrey Mieno. Toto walipata bao la kufutia machozi liliofungwa na lilifungwa na Selemani Kibuta dakika zalala salama.

Ushindi huo, umeifanya Azam ifikishe pointi 30, pointi 2 nyuma ya vinara Yanga wenye pointi 32.

Kikosi cha Azam FC kilichoshuka leo ni
1. Mwadini Ally
2. Malika Ndeule
3. Samih Haji Nuhu
4. David John Mwantika
5. Jockins Atuddo
6. Kipre Bolou
7. Brian Umony
8. Salum Abubakar
9. Abdi Kassim
10. Humhrey Mieno
11. Khamis Mcha

Post a Comment

Previous Post Next Post