DIWANI ATOA MSAADA WA CHARAHANI-NACHINGWEA

MAKALA 037Diwani wa kata ya Mkotokuyana,wilaya ya Nachingwea, Likolovele Ahamadi Asali akikabidhi msaada wa charahani kwa viongozi wa vikundi vya vijiji vya Mandai na Mkotokuyana kuunga mkono jitihada zao za kupambana na umaskini kwa vitendo.MAKALA 042Wanakikundi wa kijiji cha Mkotokuyana wakishangilia baada ya kukabidhiwa charahani na Diwani wao Likolovele Asali kwenye sherehe fupi iliyofanyika kwenye kijiji hicho.
Christopher Lilai, Nachingwea
DIWANI kata Mkotokuyana(CHADEMA), wilaya ya Nachingwea, Mkoa wa Lindi, Likolovele Ahmadi Asali ametoa msaada wa charahani mbili kwa vikundi viwili vya vijiji vya Mandai na Mkotokuyana.
Sherehe fupi ya kukabidhi chaharani hizo na mipra kwa vijana wa kata hiyo ilifanyika jana katika kijiji cha Mkotokuyana na kuhudhuria na wawakilihi wa vikundi hivyo ambao walishukuru kwa kupata vitendea kazi hizo.

Wakizungumza nje ya shehere hizo baadhi ya wananchi hao walisema kuwa upatikanaji wa vifaa hivyo itakuwa chachu katika kuongeza tija katika vikundi hivyo ambavyo kwa sasa vinajishulisha na kilimo na kuwa kupitia vifaa hivyo wataboresha kilimo chao na kuwa cha kisasa zaidi.
Awali akikabidhi charahani hizo,Diwani huyo ambaye pia ni mwenye kiti wa CHADEMA wilaya ya Nachingwea, Likolovela aliwataka wanakikundi hao kutobweteka na kutumia vifaa hivyo kama mtaji wa kukuza uzalishaji ili kuboresha hali ya maisha ya vikundi hivyo na kuvitumia kwa manufaa ya wanakikundi.
“Tumieni vifaa hivi kwa lengo la kuongeza mtaji wa kikundi ili kuboresha maisha ya kikundi na wanakikundi ili kuwaletea maendeleo na kama mtavitumia vizuri naahidi kuendelea kutoa vifaa zaidi kwa vikundi vingine ”alisema Likolovela.

Post a Comment

Previous Post Next Post