BREAKING NEWS: LULU SASA URAIANI



Habari zilizonifika hivi sasa ni kuwa msanii wa movie Lulu tayari ameshaachiwa kwa dhamana leo hii katika mahakama kuu jijini Dar. Licha ya kukamilisha kwa masharti yote aliyopewa jana ikiwa ni pamoja na  kutoa milioni 20 kwa wadhamini wawili,  kuripoti kila mwanzo wa mwezi na kuacha hati yake ya kusafiria mahakamani hapo, Lulu hakufanikiwa kutoka jana hiyo hiyo kwa kile kilichoripotiwa kutokuwepo kwa msajili wakati huo, hivyo kumlazimu kurudi gerezani

Post a Comment

Previous Post Next Post