Wenger hana nia ya kumsajili Beckham

David Beckham
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger, amepuuzilia mbali madai kuwa anapanga kumasajili aliyekuwa mchezaji wa timu ya taifa ya Uingereza David Beckham, baada ya kumruhusu mchezaji huyo kufanya mazoezi na klabu yake.
Beckham, 37, hana klabu tangu alipokihama klabu ya Los Angeles Galaxy mwisho wa msimu uliopita.
Wenger alisema, mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United alimpigia simu kuuliza ikiwa anaweza kufanya mazoezi na Arsenal.
Beckham hajacheza mechi yoyote tangu mwezi Decemba wakati alipoisaidia klabu yake ya LA Galaxy kuhidhafi kombe la MLS kwa mwaka wa pili mfululizo, kufuatia ushindi wao wa magoli matatu kwa moja dhidi ya Houstan Dynamo.
Mchezaji huyo alikuwa amehusishwa na vilabu ya Paris Saint Germain na Monaco, lakini baada ya mechi hiyo alisema kuwa hana uhakika ni klabu ipi ataichezea.
Bechkam aliicheza timu ya taifa ya Uingereza mechi mia moja na kumi na tano na mwara ya mwisho ni mechi kati ya Uingereza na Belarus Oktoba mwaka wa 2009.
- BBC

Post a Comment

Previous Post Next Post