Breaking News:Watatu wafariki dunia vurugu za Mtwara

 
Magari yakiwa yanateketea kwa moto mkoani Mtwara.
Nyumba ikiteketea kwa moto mkoani Mtwara hii leo katika vurugu zilizozuka.

WATU watatu wamefariki dunia Mkoani Mtwara baada ya kutokea vurugu kubwa kati ya Askari wa Jeshi la Polisi na waendesha Pikipiki maarufu  (Bodaboda).

Taarifa za tukio hilo zilizotufikia hivi Punde zinadai kwamba vurugu hizo zimesababishwa na Askari Poli kumkamata mmoja wa dereva bodaboda hao na kuanza kumpiga kiasi cha kupoteza fahamu.

Mbali na watu hao waliouwawa katika vurugu hizo taarifa hiyo pia imeeleza kuwa zaidi ya nyumba na ofisi tatu za serikali pamoja na magari matano yamechomwa moto.

Tunaendelea kuzifuatia taarifa hizo kwa kina na tutaendelea kuwajulisha hivyo endeleeni kufuatilia kwa undani wake.

Chanza Habarimpya.com

Post a Comment

أحدث أقدم