
SHIRIKISHO la soka barani Afrika (CAF) limetoa ufadhili kwa
Shirikisho la soka Tanzania (TFF) katika kurabati kituo chake cha michezo
kilichopo Karume jijini Dar es Salaam.
Ufadhili huo ni sehemu ya mpango wa kusaidia wanachama
wake katika dhima nzima ya kuchangia maendeleo ya soka ambapo utahusisha kukarabati maeneo mbalimbali ya mpango huo ikiwemo uwanja
na hosteli zilizopo Karume.
Tayari zimeshatangaza tenda kwa makampuni
mbalimbali ili kujitokeza kwa ajili ya kuendesha mradi huo kabla ya bodi husika
kukaa na kuteua kampuni itakayofanya ukarabati huo.
إرسال تعليق