
Waziri
mkuu mstaafu Edward Lowasa [kuli] akiteta jambo na waziri mkuu Mizengo
Pinda[kati]kushoto ni mwenyekiti mstaafu wa CCM mkoa wa Morogoro,lnjinia
Petro Kingu na aliyekluwa jirani na mawaziri hao ni mkuu wa mkoa wa
Morogoro Joel Bendera
MBUNGE wa
Monduli ambaye pia ni waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowasa anatarajiwa
kuongoza shughuli za uzindizi wa mfuko wa jamii pamoja na Tovuti ya
chama cha waandishi wa habari mkoa wa Morogoro (MOROPC) wakati wa
sherehe ya kuuaga mwaka 2012 na kuukaribisha 2013.
Hayo
yalibainishwa leo mchana na Mwenyekiti wa Muda wa Moropc Boniventure
Mtalimbo wakati akiongea na waandishi wa habari kwenye ofisi za chama
hicho, na kusema uzinduzi huo utafanyika Januari 19 mwaka huu katika
hoteli ya kitalii ya Nashera mjini Morogoro.
Mtalimbo
alisema lengo la kuanzishwa kwa mfuko wa jamii ni kuwawezesha
waandishi wahabari, kwenda vijijini kwaajili ya kuandika habari kutokana
na maeneo hayo kushindwa kufikika kwa urahisi kutokana na ukosefu
wafedha.
Aliongeza
kusema kwamba mbali na waandishi kwenda vijijini pia utakuwa ukisaidia
kwa mambo mbalimbali ikiwemo kwenye maafa, kama vile vifo, magonjwa
pamoja na kuwawezesha kujiendeleza kielimu.
Akizungumzi
uzinduzi wa tovuti (Website) alisema waandishi wa habari mkoani
Morogoro watakuwa wakiandika makala mbalimbali zikiwemo za kuelimisha
jamii,na kuandaa vipindi vya televisheni na redio na kuingiza kwenye
tovuti hiyo.
Pia
Mwenyekiti huyo aliwaomba wadau mbalimbali ndani nanje ya mkoa wa
Morogoro, kujitokeza kuchangiakwa hali na mali mfuko huo ili kuwawezesha
waandishi hao kufanya kazi kwa ufanisi zaidi pamoja na kuibua mambo
mbalimbali yaliyojificha hususani vijijini.
Aliwataja
wadhamini waliojitokeza hadi sasa kuwa ni Hoteli ya Nashera, Banki ya
CRDB, Mamlaka ya mapato Tanzania TRA,Kampuni ya Umeme ya Mac Dolnad Live
line,Kampuni ya Abood, Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini Azizi Abood,
Mamlaka ya Maji safi na Taka mkoa wa Morogoro MORUWASA.
na dustan
Post a Comment