Mwamuzi Howard Webb |
Mshambuliaji wa Livewrpool, Luis Suarez |
Kocha Alex Ferguson wa Manchester United |
Manchester, England
KOCHA
wa Manchester United, Sir Alex Ferguson anataka refa wa mchezo wao wa
leo Howard Webb amuangalia kwa jicho la karibu mshambuliaji wa
Liverpool, Luis Suarez katika mechi yao ya leo ya ligi kuu.Ferguson amemtaka Webb na wasaidizi wake kumuangalia kwa karibu mshambuliaji huyo wa Uruguay mwenye magoli 15 kwenye ligi kuu mpaka sasa.
Kocha Ferguson alisema Suarez amekuwa matukio mengi ya utata ndani ya uwanja hasa ya udanganyifu kwa waamuzi kwenye mchezo.
“Kijana anaambatana na matukio ya utata, Sijui kama anayafurahia au hapana ila ni jambo ambalo tunatumai kwamba halitatuangukia nasi na kutuathiri katika mchezo wa kesho (leo)."
Kijembe hicho cha Ferguson amekitoa siku moja kuelekea kwenye mchezo wao wa leo wa ligi kuu
Wakati Ferguson akisema hayo, Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers amedokeza matukio jinsi yalivyokwenda kinyume nao wakati walipocheza dhidi ya United mara ya mwisho na kumshuhudia Jonjo Shelvey akitolewa nje kwa kadi nyekundu ambayo anasema ilikuwa kadi ya kuonewa.
Katika mchezo huo wa ligi kuu United walishinda kwa magoli 3-2 shukrani kwa goli la penalti ya 'utata' kwenye Uwanja wa Anfield.
Rodgers alisema kuwa wanatumaini kwamba maamuzi hayatwaonea kama ilivyokuwa kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza
"Kadi nyekundu na penalti vilitugharimu kwenye mchezo ule, natumai hawatapata maamuzi ambayo yatachangia matokeo," alisema Rodgers.
Wapinzani hao wa ligi kuu wanakutana leo kwenye uwanja wa Old Trafford kwenye mchezo unaotarajiwa kuwa na upinzani mkubwa.
Post a Comment