SIKU chache baada ya kifo cha mwigizaji Juma Kilowoko, mwigizaji
Jacqueline Wolper amefungukia uhusiano wake na marehemu hadi kufikia
hatua ya kuchangia kiasi cha shilingi milioni 15 kwa ajili ya matibabu.
Akizungumza na Funguka na Risasi kwenye msiba wa msanii huyo pande za Tabata Bima jijini Dar, Wolper alisema Sajuki alimpenda kama kaka yake wa damu ndiyo maana alikuwa tayari kumsaidia kwa hali na mali.
Akizungumza na Funguka na Risasi kwenye msiba wa msanii huyo pande za Tabata Bima jijini Dar, Wolper alisema Sajuki alimpenda kama kaka yake wa damu ndiyo maana alikuwa tayari kumsaidia kwa hali na mali.
“Kila mmoja alinishangaa nilipotoa shilingi milioni 15 kwa ajili ya gharama za matibabu ya marehemu. Ukweli ni kwamba marehemu nilimpenda kama kaka yangu wa damu.” alisema Wolper huku akibubujikwa na machozi.
Funguka: “Kwa nini ulimpenda kiasi hicho? Kwani huna kaka zako wa damu mpaka upendo wako uuelekeze kwa Sajuki?
Wolper: (Anafuta machozi na kuongea kwa huzuni)“Kaka wa damu ninao, ila Sajuki nimechipukia naye katika tasnia ya sanaa ya maigizo na alikuwa na upendo wa kweli kwa kila mtu, hakupenda kubeba mambo ya ajabu moyoni mwake na alikuwa mwepesi wa kukubali ushauri wowote unaompa.”
Funguka: “Sababu hizo tu ndiyo zikufanye kumpenda kiasi hicho, kwani hakuna wasanii wengine wenye moyo kama wa Sajuki”?
Wolper: “Wapo lakini hata katika familia yenu mnaweza kuwa mmezaliwa watoto watano ila kati ya hao ukampenda mmoja kuliko wengine. Hiyo huwa inatokea.”
Funguka: “Sajuki ndiyo hatuko naye tena, upendo wako utauelekeza kwa msanii gani?”
Wolper: (Machozi yakamtoka na kutaka aachwe kidogo, kisha akajikaza na kusema) “Marehemu ameacha mjane na mtoto mmoja.
“Upendo wangu nitauelekeza kwa mkewe Wastara pamoja na mwanaye kwani natambua msanii mwenzangu kwa sasa ana pengo kubwa la kuondokewa na mzazi mwenzake, sipo radhi kumuona akiwa mpweke.”
Funguka: “Ina maana kabla ya kifo cha Sajuki ulikuwa huna upendo na Wastara?”
Wolper: “Hapana, niliwapenda wote tena kwa moyo wa dhati ndiyo maana nilikuwa natumia muda wangu mwingi kuhakikisha Sajuki anapona.
Funguka: “Licha ya kuwa karibu sana na marehemu ni jambo gani umejifunza kutoka kwake ambalo huwezi kulisahau maishani?”
Wolper: “Upendo aliokuwa nao kwa mkewe Wastara umenipa darasa kubwa sana. Ina maana kuwa mkishapendana hata kama mtapatwa na matatizo makubwa kiasi gani, mkimtegemea Mungu maisha yanasonga mbele.
“Maisha ya Sajuki na Wastara yalianza kupata mikosi tangu wakiwa wachumba. Nakumbuka Machi 12, 2009 walipata ajali mbaya ya ‘bodaboda’ maeneo ya Tabata, Dar. Katika ajali hiyo Wastara alivunjika mguu na watu wengi wakajua kuwa Sajuki atamtosa na kuchukua msichana mwingine lakini mambo hayakuwa hivyo.
“Hakika huo ni upendo wa dhati ambao ni wanaume wachache wenye moyo wa huruma kama aliokuwa nao marehemu. Mbali na hilo tangu waoane mwaka 2009 ndoa yao imekuwa na changamoto za hapa na pale lakini hawakuachana.”
Funguka: “Nikuache upumzike, tupo pamoja katika kipindi hiki kigumu.”
Wolper: “Asante sana kaka.”
Post a Comment