Ghana na Mali zatinga hatua ya Robo DRC na Niger njee kwenye mashindano

Nahodha wa Ghana Asamoah Gyan akishangilia goli na Kiungo wake Emmanuel Agyemang Badu
Na Nurdin Selemani Ramadhani

Timu ya Taifa ya Ghana maarufu kama Black Stars imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali baada ya kufanikiwa kumaliza kinara wa Kundi B kutokana na ushindi ambao waliupata dhidi ya Niger. Ghana wameibuka na ushindi mnono wa magoli 3-0 mbele ya Niger na hivyo wamefanikiwa kupata tiketi ya kucheza na Cape Verde katika mchezo wa hatua ya robo fainali.


Nahodha Asamoah Gyan ndiye alipachika goli la kwanza kabla ya Christian Atsu na John Boye kufunga magoli mengine ambayo yakaisadia Ghana kusonga mbele katika hatua ya robo fainali.

Ghana wamepata ushindi huo kutokana na kucheza soka ya kuvutia hatua ambayo imewafanya mashabiki wao kushangilia muda wote baada ya kukata tiketi ya kuingia kwenye nane bora.

Kundi B pia limeshuhudia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ikiondolewa kwenye mashindano kufuiatia kupata sare ya goli 1-1 dhidi ya Mali ambayo imepata tiketi ya kutinga robo fainali.

DRC ndiyo walikuwa wa kwanza kufunga goli kupitia mkwaju wa penalti iliyokwamishwa nyavuni na Dieumerci Mbokani kitu ambacho kilitoa matumaini ya Congo kuweza kusonga mbele lakini matumaini yao yakapotea.

Dakika kumi na moja baadaye Mali walisawazisha kupitia Mahamadou Samassa na hivyo kujipatia pointi moja baada ya sare dhidi ya DRC na hivyo watacheza na wenyeji Afrika Kusini maarufu kama Bafana Bafana kwenye robo fainali.

Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika yataendelea kwa michezo miwili ya Kundi C ambapo Burkina Faso watapambana na Zambia huku Ethiopia watakuwa na shughuli dhidi ya Nigeria.

Via kiswahili.rfi.fr

Post a Comment

أحدث أقدم