Binti wa miaka 20, Shanteli Rusike, raia wa Zimbambwe Mkesha wa X Mass
haukuwa mzuri kwake kwani alikamatwa na kuwekwa ndani kutokana na ku
share picha inasemekana kumdhalilisha raisi wa nchi hiyo, Robert Mugabe.
Tukio hilo lilimkuta binti huyo ambaye aliikuta picha hiyo katika
mtandao na kuanza kuwasambazia rafiki zake ambao baadhi yao
walikasirishwa na kitendo hicho na kuamua kumripoti polisi. Kesi yake
ipo mahakamani na yupo nje kwa dhamana ya dola 100 za kimarekani. Miaka 5
iliyopita, kijana mwingine wa nchi hiyo alikutwa na picha kama hiyo na
kutumikia miezi minne gerezani.
إرسال تعليق