Hofu ya nchi kuporomoka Misri

Kamanda mkuu wa majeshi nchini Misri ameonya kuwa mgogoro wa sasa wa kisiasa huenda ukasababisha nchi kuporomoka
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Generali Abdel Fattah al-Sissi, alisema kuwa ikiwa hali hiyo itatokea , huenda ikaathiri pakubwa vizazi vijavyo.
Aitoa matamshi yake baada ya idadi kubwa ya wanajeshi kupelekwa katika miji mitatu.
Zaidi ya watu 50, wamefariki katika siku kadhaa za maandamanmo na ghasia.
Matamshi ya Generali, Sissi yametafsiriwa kama kitisho kwa waandamanaji na upinzani pamoja na kuwa wito wa utulivu kwao. Pia ni kuwahakikishia wananchi kuhusu jukumu la jeshi.
Maandamano ya ghasia yemeendelea usiku kucha nchini Misri, huku maelfu ya waandamanaji wakikiuka sheria ya kutotoka nje katika baadhi ya miji iliyowekwa na Rais Mohammed Morsi pamoja na sheria ya hali ya hatari.
Idadi kubwa ya watu wameuawa katika mandamano ya siku tano zilizopita na ambayo yalikumbwa na vurugu.
Upinzani Misri umekataa mwaliko wa Rais Moris wa mazungumzo ya kitaifa
Maelfu ya waandamanaji walimiminika katika mitaa ya miji ya Misri ya Suez, Port Said, na Ismailiya kupinga amri ya kutotoka nje iliyowekwa na Rais Mohamed Morsi.
Mtu mmoja ameuawa kwa kupigwa risasi katika mji wa Port Said ambako waandamanaji waliwashambulia polisi.
Bwana Morsi alitangaza hali ya tahadhari na amri ya kutotoka nje Jumapili ili kukabiliana na maandamano ya ghasia, ambayo hadi sasa yamesababisha vifo ya watu 50
Maelfu ya askari wamewekwa kushika doria. Wakati makabiliano yakiendelea mjini Cairo ,chama rasmi cha upinzani kimekataa mwaliko wa Rais wa mazungumzo ya kitaifa .
Wakati huo huo baraza la Misri la bunge- Ashura- -limebuni sheria inayopatia wanajeshi mamlaka ya kutia nguvuni mtu yeyote anayekiuka amri.
Wito uliotolewa na Rais Morsi wa mazungumzo ya kitaifa, umepuuziliwa mbali na wapinzani wake.
Aliwataka viongozi wa upinzai, kuhudhuria mkutano siku ya Jumapili jioni katika juhudi za kutuliza hali ya hasira lakini ni washirika wa wake pekee waliofika kwa mkutano huo.
Maandamano ya hivi punde katika miji hiyo, yamechochewa na adhabu ya kifo iliyotolewa kwa mashabiki 21 wa soka waliohusika na ghasia
Kundi kubwa zaidi la upinzani nchini Misri limesema halitahudhuria mazungumzo yanayoandaliwa na Rais Mohamed Morsi hadi pale masharti yatakapotimizwa.
Mkutano huo ulinuia kumaliza machafuko ambayo yamekuwa yakiendelea katika miji kadhaa katika siku za hivi karibuni.
Awali Rais Morsi alitangaza hali ya hatari ya muda wa mwezi mzima katika miji ya Port Said, Suez na Ismailiya kufuatia siku kadhaa ya maandamano na fujo.
Amesema kuwa pia ameweka amri ya kutotoka nje usiku kucha. Kiongozi wa kundi la upinzani la Free Egyptians Party, Dr Ahmed Saeed, ameaimbia BBC kuwa rais Mosri anapaswa kufanya juhudi zaidi kurejesha imani ya wananchi.
Serikali ya rais Morsi inakabiliwa na upinzani mkali
Mapema leo Rais wa Misri Mohammed Morsi ametangaza hali ya tahadhari katika miji ya Port Said, Suez na Ismalia baada ya siku kadhaa za machafuko makali.
Kuanzia Jumatatu na kwa siku 30 zijazo watu hawatakubaliwa kutoka nje kati ya saa 21:00 na 06:00, alisema alipohutubia taifa.
"Huwa kwa kawaida napinga hali za tahadhari, lakini ilibidi niwalinde wananchi na kukomesha umwagikaji damu basi ikanabidi nifanye hivyo,” rais alisema.
Takriban watu 33 people walikufa mwishoni mwa wiki huko Port Said, ambapo uamuzi wa mahakama ulisababisha vurugu kuzuka.
Kutoridhika na uongozi wa Bwana Morsi's kulizua fujo kwingine nchini.
Katika mji mkuu wa Cairo, waadamanaji wailokuwa wanaipinga serikali walipambana na vikosi vya ulinzi karibu Uwanja wa Tahrir kwa siku ya nne mfululizo.

Upinzani

Upinzani unamlaumu Morsi kwa kutawala kimabavu na kuipa kipaumbele katiba mpya ambayo hailindi kikamilfu haki za kuabudu wala za maoni.
Serikali pia imelaumiwa kwa kutodhibiti hali ya uchumi, inayozidi kuzorota.
Bwana Morsi alisema kwamba angechukua hatua zaidi "kwa ajili ya Misri" na kwamba ilikuwa "wajibu wake" kama rais kufanya hivyo.
Vuru katika mji wa Portland
Aidha, aliwaalika viongozi wa kisiasa wakutane "katika majadiliano ya kitaifa " mnamo Jumatatu.
Ingawaje muungano mkubwa zaidi wa vyama pinzani nchini Misri, National Salvation Front, uliuunga mkono mualiko huo, ulilaumu sera za Morsi kwa kuzua vurugu.
Vurugu zilizuka Port Said baada ya mahakama kuwahukumu watu 21 kifo kwa kuhusika na fujo baada ya mechi ya kandanda Februari 2012.
Chanzo:- BBC Swahili

Post a Comment

Previous Post Next Post