Gazeti la taifa nchini China
limeonya kuwa Beijing haitasita kukomesha msaada kwa Korea Kaskazini
ikiwa itafanya jaribio lengine la kinuklia.
Taarifa kwenye gazeti hilo, Global Times,
inajiri baada ya Kaorea Kaskazini kujibu vikali hatua ya kuwekewa
vikwazo vikali zaidi dhidi yake na Umoja wa Mataifa mwezi jana.China ni mshirika mkubwa wa Korea Kaskazini,
Pia inaarifiwa kuwa China inataka uthabiti katika rasi ya Korea lakini haitakuwa mwisho wa dunia ikiwa mgogoro mdogo utaibuka.
Korea Kaskazini imeonya vikali Korea Kusini dhidi ya kujihusisha na vikwazo hivyo vya Umoja wa Mataifa.
إرسال تعليق