
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi aka Sugu kesho anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa internet cafe ya rapper Emmanuel ‘Izzo B’ Simwinga.
Ofisi hiyo iitwayo Izzo Bizness Internet Cafe & Secretarial Bureau ipo TEKU University jijini Mbeya.
Akiongea na mtandao huu , Izzo amesema katika uzinduzi huo utakaoanza saa 8 mchana hakutakuwa na performance yoyote bali watafungua champagne za kutosha.
"Kesho mungu akisaidia ntafanya ufunguzi rasmi
wa Internet cafe yangu iliyopo MBEYA chuo Cha Teofilo kisanji(TEKU) NA
Mgeni rasmi atakuwa MH:Joseph mbilinyi mbunge wa mbeya...
Kama uko MBEYA na unataka kushuhudia uzinduzi
wa ufunguzi wa Internet cafe yangu iliyopo chuo Cha teku MBEYA
utakaofanywa na Mh: Joseph Mbilinyi mbunge wa MBEYA Mjini unaweza kuja hakuna
kiingilio muda ni saa Nane Mchana...karibuni".....Izzo b
إرسال تعليق