JOTO LA UCHAGUZI: POLISI WAMKAMATA MTU MMOJA KWA MATUMIZI MABAYA YA FACEBOOK


Wakati Kenya inazihesabu siku kadhaa kufikia siku ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo, serikali ya Kenya inajaribu kwa njia zote kuziba mianya yote inayoweza kuzua hali ya machafuko kama yale yaliyotokea baada ya uchaguzi mwaka 2007, na sasa wameangazia facebook na blogs zinazohatarisha hali ya usalama.

Masaa machache baada ya serikali ya Kenya kutoa onyo kwa watumiaji na waendeshaji wa facebook pages na blogs kwa kuandika speeh ama status za uchochezi, mapema jana wamemkamata administrator wa moja kati ya facebook pages tano ambazo zilitajwa katika list ya kupewa onyo na serikali hiyo .

Admin huyo wa fan page maarufu ya "Gor Mahia is Not a Club, Its a Lifestyle. But do we say", Collins Okello a.k.a Dr. Jarunda Jaluth Mambodiad alikamatwa na kupelekwa katika makao makuu ya polisi kitengo cha upelelezi (CID) kwa ajili ya mahojiano ya kina kuhusu status za uchochezi kwenye page yake .

Hata hivyo, kwa mujibu wa chanzo kimoja cha kuaminika, Collins aliachiwa baada ya mahojiano hayo. Lakini baada ya kufungwa kwa fan page hiyo, imeanzishwa upya fan page nyingine yenye jina hilohilo "Gor Mahia is Not a Club, Its a Lifestyle. But do we say," na hadi sasa ina LIKE zaidi ya 4, 340, ikiwa ni masaa 20 hivi baada ya kufunguliwa huku ikidrop status inayozungumzia kufungwa kwa original fan page yao...

hii ni moja kati ya status hizo katika page hiyo..

"Jarunda was forcefully compelled to delete the original page".

Kwani ukiwa CORDed ni hate speech.
Mbona page ya Stop Raila, RIP Sk Macharia etc hazijafungwa.

We are condeming this intrusive movement of the govt, oppressing the weak n poor, inflicting fear in them intentionally to deprive them their constitutional rights...anyone is free to talk sense..."

Post a Comment

أحدث أقدم