Baada ya miaka kadhaa ya kutokuwa na ushirikiano wa kidiplomasia kati
ya kenya na somalia, kenya sasa imechukua hatua ya kwanza kuanzisha
uhusiano huo kwa kufungua ubalozi wake mogadishu katika mji mkuu wa
somalia.
Balozi wa kenya mtarajiwa josephat maikara tayari amewasilisha vyeti
vyake kwa rais wa somalia, hassan sheikh mahmoud. Rais mahmoud
aliikaribisha hatua hii ya kenya akisema itasaidia katika kutatua
maswala mengi ya kiusalama katika mpaka wa nchi hizi mbili.
Uturuki ndio ilikuwa nchi ya kwanza akufungua ubalozi wake somalia
miaka miwili iliopita. Tangu hapo libya, iran na misri zimefuata nyayo.
October 2011, majeshi ya kenya yaliingia somalia kukabiliana na kundi la
kigaidi la al-shabaab. Wanamgambo wa al-shabab wametishia kuwaua mateka
wote raia wa kenya, katika wiki tatu zijaazo, iwapo serikali ya kenya
haitawaachilia huru wapiganaji wake wanaowazuiliwa. Al-shabab walimuua
raia mmoja wa ufaransa waliokuwa wanamshika mateka kwa zaidi ya miaka
mitatu, pale operesheni ya kumuokoa ilioendeshwa na maajasusi wa
ufaransa ilipotibuka.
Post a Comment