Kenya yafungua ubalozi Somalia [video]


Baada ya miaka kadhaa ya kutokuwa na ushirikiano wa kidiplomasia kati ya kenya na somalia, kenya sasa imechukua hatua ya kwanza kuanzisha uhusiano huo kwa kufungua ubalozi wake mogadishu katika mji mkuu wa somalia.
Balozi wa kenya mtarajiwa josephat maikara tayari amewasilisha vyeti vyake kwa rais wa somalia, hassan sheikh mahmoud. Rais mahmoud aliikaribisha hatua hii ya kenya akisema itasaidia katika kutatua maswala mengi ya kiusalama katika mpaka wa nchi hizi mbili.
Uturuki ndio ilikuwa nchi ya kwanza akufungua ubalozi wake somalia miaka miwili iliopita. Tangu hapo libya, iran na misri zimefuata nyayo. October 2011, majeshi ya kenya yaliingia somalia kukabiliana na kundi la kigaidi la al-shabaab. Wanamgambo wa al-shabab wametishia kuwaua mateka wote raia wa kenya, katika wiki tatu zijaazo, iwapo serikali ya kenya haitawaachilia huru wapiganaji wake wanaowazuiliwa. Al-shabab walimuua raia mmoja wa ufaransa waliokuwa wanamshika mateka kwa zaidi ya miaka mitatu, pale operesheni ya kumuokoa ilioendeshwa na maajasusi wa ufaransa ilipotibuka.

Post a Comment

أحدث أقدم