TUKIO la hivi karibuni la mwandishi wa habari wa Radio Kwizera, Issa
Ngumba (pichani) kukutwa amekufa huku akiwa amenyofolewa sehemu zake za
siri limewasikitisha wengi huku ushirikina ukitajwa.
Wakizungumza na mwandishi wetu kwa nyakati tofauti, baadhi ya wakazi wa eneo la Kakonko ambako ndiko marehemu alikokuwa akifanyia kazi walisema, tukio hilo ni la kinyama na kuna uwezekano wahusika wamechukua sehemu nyeti na kwenda kuzifanyia mambo ya kishirikina.
“Kwa kweli ni kifo kinachoumiza sana ila ninachoamini ni kwamba, hawa wahusika wamezichukua nyeti hizo kwenda kufanyia mambo ya kishirikina lakini Mungu atasimamia zoezi la kuwapata, naamini polisi watafanya kazi yao vizuri,” alisema Saleh Idd aliyekuwa akimfahamu marehemu.
Ngumba alipotea tangu Januari 5, mwaka huu majira ya saa 11 jioni ambapo alimuaga mkewe Bi. Rukia Yunus kuwa anatoka kidogo lakini hakuweza kupatikana hadi Januri 8 mwili wake ulipopatikana nje kidogo ya mji wa Kigoma akiwa amefariki dunia.
Tunaipa pole familia ya marehemu na linaliomba jeshi la polishi kuharakisha uchunguzi wa kifo cha mwanahabari huyo na ikiwezekana kuwapata waliohusikka na kifo hicho.

Post a Comment