NEW YORK, Marekani
KUNDI la
muziki lilowahi kutamba hapo nyuma la Destiny's Child limetangaza kurejea upya
likiwa pamoja ambako wanatarajia kuachia albamu yao mpya itakayokwenda kwa jina
la ‘Nuclear’.
Kundi hilo
la muziki wa R&B lilitoa taarifa hiyo juzi baada ya kukaa kimya tangu mwaka
2004 ambako ndipo walitoa albamu yao ya mwisho na kila mmoja kutawanyika na
kufanya kazi binafsi.
Albamu ya ‘Nuclear’
inatarajiwa kuwa na nyimbo 13 ambazo ziliwahi kutamba hapo nyuma kama vile ‘Emotion’
na ‘Cater 2 U’ na baadhi ya kazi mpya ambazo zinatarajiwa kuwemo ni pamoja na ‘Love
Songs’ inayotarajiwa kutoka Januari 29.
Kazi hiyo ya
‘Nuclear’ imetengenezwa chini ya utayarishaji wa Pharrell, akiwa ameshirikiana
na mwimbaji Michelle Williams.
Destiny's
Child, inaundwa na waimbaji kama vile Williams, Beyonce Knowles na Kelly
Rowland ambao walifanikiwa kutikisa ile mbaya katika anga za muziki na kuushtua
ulimwengu lakini baadaye kukaibuka malalamiko kutoka kwa weaimbaji wengine
wakilaumu kwamba nafasi kubwa anakuwa anapewa mwimbaji Beyonce kwa sababu
mkurugenzi wao alikuwa baba mzazi wa mwimbaji huyo.
Post a Comment