NDIKUMANA HALI MBAYA

MSAKATA kabumbu mkali nchini Rwanda ambaye pia ni mume wa diva wafi lamu za Kibongo, Irene Uwoya, Hamad Ndikumana ‘Katauti ’ ni mgonjwa kiasicha kushindwa kuendelea kuichezea timu yake ya Rayon Sports ya Rwanda.
Akiwasiliana na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya mtandao wa kijamii wa ‘Facebook’,Ndikumana alisema kuwa kwahivi sasa hali yake siyo nzuri kiafyana ndiyo maana ameshindwa kujiunga na mazoezi ya timu yake hiyo.
“Kwa hivi sasa bado naumwa,hivyo sija ichezea timu yangu mchezo wowote mpaka afya yangu itakapo imarika,” alisema Ndikumana.
Ndikumana akiwa na Irene Uwoya enzi za mapenzi yao
Hata hivyo, Ndikumana hakuweka wazi ugonjwa ambao unamsumbua ingawa hivi karibuni aliweka picha kwenye mtandao huo akidai kuwa ametolewa kitu kama pembe kwenye mwili wake baada ya kuhangaika kwa muda mrefu kupata tiba.
Mwanasoka huyo aliyekuwa akisakatasoka la kulipwa nchini Cyprus aliingia
kwenye mgogoro wa ndoa na mkewe akiwa Tanzania na kuamua kurejea nyumbani kwao Rwanda mwaka jana

Post a Comment

Previous Post Next Post