Maandalizi makubwa yafanyika jijini Washington DC kwa Sherehe za
kuapishwa kwa Rais wa Marekani Barack Obama yameanza kukamilika.
Vyombo
vya Habari mbali mbali hapa nchini Marekani vimekuwa katika kukamilisha
matayarisho ya kupata matukio ya kuapishwa Rais Barak Obama kwa muhula
wa Pili Ikiwa Mmarekani wa kwanza mwenye asili ya Kiafrika kuchaguliwa
kwa mara ya pili na hivyo kuifanya sherehe hiyo kuwa ya Kihistoria.
Sherehe
hizo zitafanyika katika viwanja vya National Mall na Memorial Parks
zitahudhuriwa na mamilioni ya Raia wa marekani na wageni kutoka nchi
mbali mbali kote ulimwenguni.
Rais Obama wa Marekani alichaguliwa
kwa kura nyingi baada ya kumshinda mgombea wa kiti cha chama cha
Republican Mitt Romney na kuingia awamu ya pili ya Urais ya Urais wa
Marekani
Karibia mwenzi mzima ufundi wa maandalizi ya Obama inauguration 2013
yaliokua yakifanyika katika maeneo mbali mbali ya Jijini Washington DC
yaaza kutia Sura, hapa ni Jengo la Congress ya Marekani Jijini
Washington DC.

Baadhi ya ufundi uliokamilika katika jingo la Capitol Hill liliopo
washington DC na viti vilivyopangwa rasmi kwa ajili ya wageni wanunuzi
watikiti za 2013 Inauguration History ndio makazi yao yatakapokua hapa
kwa siku ya Jumatatu Jan. 21, 2013 (Picha zote na
swahilivilla.blogspot.com)

Cheif wa swahilivilla blog Abou Shatry akipata picha ya 2013 katika
jingo la Congress ya Marekani liliopo washington DC katika jingo la
Capitol Hill liliopo down town Washington DC Nchini Marekani.

Picha 2008 Inauguration History: Hivi ndivyo itakavyokua Siku ya
Jumatatu Januwari 21, 2012 kwenye Jumba la Congress ya MarekaniDown Town
Washington DC.

Sehemu kubwa ya sherehe ya kuapishwa kwa rais Obama ikifanyiwa ukarabati wamuda.
Rubber floor tiles zikitandazwa maeneo ya sakafu zilizokua na mchanga
kwaajili ya kuhifadhi tope tope zisitimke na kuharibu eneo hilo kubwa la
National Mall,

Kukanyaga mchanga Marekani ni kosa kubwa na ndio maana wameweka Rubber
floor tiles kwaajili ya kukanyagia ili kunusuru michimbuko ya tope tope
na kutoshafua barabara kwa msongamano wa watu watakaomiminika kutoka
Nchi mbali mbali kuja kushuhudia kuapishwa kwa Obama

Sehemu iliotandikwa Rubber floor tiles: Hivi ndivyo Rubber floor tiles
zinavyotandikwa kwenye michanga ili kunusuru topetote raia wasichafuwe
maeneo ambayo bado yanafanyiwa ukarabati sehemu ya National Mall Jijini
hapa. Kwa picha zaidi tembelea Swahilivilla.blogspot.com
إرسال تعليق