Watuhumiwa wa Ubakaji nchini India wakiwa kwenye gari wakiingia katika mahakama inayosikiliza kesi yao. Picha Reuters/Stringer |
Mahakama Kuu nchini India imetupilia mbali ombi
lililowasiliswa na upande wa utetezi la kutaka kuhamisha kesi
inayowakabiliwa watuhumiwa watano wa mauaji, utekajinyara na ubakaji wa
mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Udaktari kutoka Jiji la New Delhi.
Jopo la majaji watatu ambao walikuwa wanasikiliza shauri la
kutaka kuhamishwa kwa kesi hiyo wameamua kulitupilia mbali kutokana na
kutoridhishwa na hoja ambazo zimekuwa zikitolewa na wanasheria wa
watuhumiwa hao.
Mahakama Kuu nchini india imekataa ombi hilo baada ya kutoridhishwa
na hoja ambazo zimewakilishwa na upande wa utetezi kitu ambacho
kinafanya kesi hiyo iendelee kusikilizwa katika Jiji la New Delhi.
Mwanasheria wa mmoja wa mtuhumiwa wa kesi hiyo Manohar Lal Sharma
ndiye aliwakilisha ombi la kutaka kubadilishwa kwa Mji ambao utumike
kusikiliza kesi hiyo akihofia kutopata haki.
Mwanasheria Sharma aliamua kuwasilisha ombi hilo kutokana na kuona
shinikizo kumbwa ambalo limekuwa likitolewa katika usikilizaji wa kesi
hiyo kitu ambacho kilimsukuma kuona haki haitopatikana kwa mteja wake.
Kesi hiyo ambayo imehamishiwa katika Mahakama inayosikiliza kesi kwa
haraka katika Jiji la New Delhi inatarajiwa kuendelea kusikilizwa baada
ya shauri hilo kutupwa na Mahakama Kuu.
Kesi hiyo imekuwa ikifuatiliwa kwa karibu na wanaharakati pamoja na
wananchi wa taifa hilo ambao wamekuwa wakitaka wabakaji hao kama
wakikutwa na hatia basi inabidi wahukumiwe adhabu ya kifo.
إرسال تعليق