Waislamu
wenye itikadi kali wanaojiita walinzi wa dini, Ansar Dine, waliudhibiti
mji wa Gao kaskazini mwa Mali kwa muda wa nusu mwaka. Baada ya
kuwatimua washirika wao wa hapo awali, waasi wa Tuareg, wapiganaji wa
Ansar Dine walianza kuzitumia sheria za Kiislamu.
Lakini
sasa watu katika mji wa Gao na mingine ya kaskazini mwa nchi hiyo
wameanza kupata utulivu baada ya wapiganaji hao wa Kiislamu kutimua mbio
kufuatia mashambulizi ya ndege za Ufaransa.
Licha
ya hisia za faraja kuonekana miongoni mwa wakaazi hao wa kaskazini,
hata hivyo watu hao pia wana wasiwasi, kwa sababu mgogoro wa nchi yao
bado haujamalizika licha ya hatua za kijeshi zinazochukuliwa na
Ufaransa.
“Sasa
hali ni shwari. Watu wanatoka majumbani mwao kuvuta sigara nje bila ya
usumbufu. Hata hivyo, muda mfupi uliopita ndege zilishambulia karibu na
hapa. Lakini hakuna raia yeyote aliyedhurika. Baadhi ya wapiganaji wa
Kiislamu bado wapo, lakini hawatoki nje ya magari yao,” anasema mmoja wa
wakaazi hao.
إرسال تعليق